UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa hawatakuwa na huruma mbele ya Simba kesho uwanja wa Uhuru ambapo utakuwa mchezo wao wa kwanza msimu huu.
Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema kuwa maandalizi yao yamekamilika na wana imani ya kubeba pointi tatu muhimu zitakazowaweka kwenye nafasi nzuri.
"Tunajua utakuwa mchezo mgumu kwa kuwa tunacheza na timu ngumu ila hiyo haitupi taabu kwa sababu na sisi pia ni wagumu.
"Wachezaji wote wana ari na morali kubwa ya kupambana na wapinzani wetu,kila kitu kitakuwa sawa na hakuna kingine tunachohitaji zaidi ya pointi tatu," amesema Katwila.
Mtibwa ipo nafasi ya tano ikiwa na pointi 49 baada ya kucheza michezo 35 imebakiwa na michezo mitatu kukamilisha ligi msimu huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment