May 22, 2019

MSHAMBULIAJI wa Yanga Heritier Makambo leo ameiongoza timu yake kushinda bao 1-0 dhidi ya Mbeya City mchezo wa ligi uliochezwa uwanja wa Uhuru.

Bao la Makambo lilipachikwa kimiani dakika ya 25 baada ya krosi safi iliyopigwa na Haji Mwinyi iliyomkuta Makambo ndani ya 18 na kumalizia kwa kichwa.

Makambo anafikisha jumla ya mabao 17 kwa sasa kwenye msimamo wa ufungaji akiwa nafasi ya pili nyuma ya Meddie Kagere mwenye mabao 23.

Ushindi huo unaifanya Yanga kujikita nafasi ya pili ikiwa na pointi zake 86 na wamebakiwa na mchezo mmoja mkononi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic