May 22, 2019



Mwekezaji wa Simba Bilionea, Mohammed Dewji ameahidi kuwazawadia pikipiki za aina ya boxer wachezaji wake wote baada ya kuipa Ubingwa wa Ligi Kuu Bara.


Kauli hiyo aliitoa jana mara baada ya timu hiyo Jana kutangaza ubingwa huo kwa kuwafunga Singida United mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Namfua, Singida.


Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mo alisema zawadi hiyo ya boxer aliyoitoa ni sehemu ya ahadi yake aliyoitoa hivi karibuni baada ya kufanya kikao na wachezaji hao 
"Hizi boxer nimezitoa mimi binafsi na siyo Simba, kabla ya kuchukua ubingwa wa ligi niliwaahidi kuwapa boxer hizo.


" Boxer hizo mimi ndiye ninayeziuza ambazo kila moja thamani yake ni Shilingi Milioni 2.4.


"Boxer hizo nimewapa kwa ajili ya kufanya biashara kwa kuwapa ndugu zao ili wajiongezee kipato ambacho kwa siku wakipata Shilingi 15, 000 siyo mbaya," alisema Mo.

5 COMMENTS:

  1. Duhh!!!! naona jina la Simba bodaboda litachukua nafasi

    ReplyDelete
  2. Usije shangaa kusikia mtu akitaka kumwita bodaboda ukasikia anaita Simba!!!!

    ReplyDelete
  3. Ati wanamuusia Ajib asiondoke Yanga anarejea kwao Kwa asili

    ReplyDelete
  4. Nani asieitaka pepo hiyo? Ati fikiri mara mbili kabla kurejea simba

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic