May 22, 2019


Aliyoyazungumza Mwekezaji Mkuu wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji Mo leo haya hapa

Niwapongeza na kuwashukuru wachezaji wamejitolea kwa namna moja au nyingine hadi tunaupata huu ubingwa, niwashukuru wanachama na wapenzi wote wa Simba kwa kujitokeza kutushangilia."- Mo Dewji
.
"Kocha ameshafikia malengo tuliyomuwekea tulikuwa tunataka ubingwa na kufika kwenye makundi ya Ligi ya Mabingwa, Mungu akitujalia kwenye wiki moja tutakaa nae tumuongeze mkataba ... tutamueleza sehemu ambazo kuna mapungufu ili aendelee kufanyia kazi"- Mo Dewji
.
"Tunaanza kupanga maandalizi ya msimu, mimi binafsi naongea na timu za Ulaya na Marekani... kuna rafiki yangu anamiliki DC United nimeongea nae watualike tukafanye maandalizi Marekani, kuna uwezekano wa kwenda Ureno, kwenye wiki mbili zijazo tutajua timu itakwenda wapi"- Mo Dewji
.
"Kwenye mechi ambayo tutacheza kesho naomba niwashukuru sana SportPesa, hii ni mara ya kwanza kwa timu kutoka ligi kuu ya Hispania kuja kucheza Tanzania, ni historia kubwa kwa nchi yetu, tupo tayari kucheza na Sevilla, naomba mashabiki tujitokeze kwa wingi sana"- Mo Dewji
.
"Simba itakuwa kwenye soko kushindana na Al Ahly, Zamalek, TP Mazembe kushindana kutafuta wachezaji wenye vipaji, tupo tayari kuwabakisha wachezaji ambao mwalimu atapendekeza, wengine watatoka kwa mkopo ... bajeti ya mwaka huu itakuwa kubwa kuliko mwaka jana"- Mo Dewji
.
"Katika mechi ya kesho ya Sevilla nawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi ili na sisi tuweze kuwaonyesha mpira wa Ulaya"- Mwenyekiti wa klabu, Swedi Mkwabi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic