May 31, 2019


KOCHA wa Mkuu wa Simba, Patrickk Aussems amesema kuwa kuelekea kukisuka kikosi chake upya msimu ujao anaongeza mashine tano za kimataifa huku akiwa na mpango wa kuwaodoa watano wengine waliopo ndani ya kikosi hicho.

Aussems amesema kuwa ili kusajili wachezaji wa kigeni wengine ni lazima kuwapunguza wale wa nje waliopo kwa sasa ndani ya kikosi.

"Kwa sasa ninataka kuwasajili wachezaji wanne au watano kwa ajili ya msimu ujao na hao watakuwa ni wa kimataifa na wenye uzoefu kwenye michuano ya kimataifa sio wale ambao watakuwa ni wageni kwenye michuano hiyo hawawezi kunisaidia," amesema Aussems.

Imeelezwa kuwa kwenye ripoti ya kocha ambayo inahitaji kusajili nyota wake wapya miongoni mwa nyota hawa panga linawahusu kutokana na sababu zilizotajwa.

Zana Coulibaly, raia wa Burkina Faso imeleezwa  ameshindwa kumudu kasi ya Simba na ushindani ndani ya kikosi.

Asante Kwasi, beki huyu wa Simba raia wa Ghana imeelezwa kuwa majeruhi yememfanya asiwe bora msimu huu na kucheza mechi chache chini ya kiwango.

Juuko Murshid, beki huyu tegemeo ndani ya kikosi cha timu ya Taifa ya Uganda hana furaha ndani ya kikosi cha Simba.

Haruna Niyonzima, imeelezwa kuwa kiungo huyu fundi raia wa Rwanda, mbelgiji anamkubali sana ila ni jeuri ndani ya kikosi cha Simba.

Emmanuel Okwi, imeelezwa kuwa nyota huyu wa timu ya Taifa na kipenzi cha mashabiki wa Simba ameomba kuachwa msimu ujao ili akajaribu changamoto mpya msimu ujao.


3 COMMENTS:

  1. panga linawahusu kwa kuwa ni jeuri ndani ya simba , na mwingine hana furaha ndani ya Simba!mwandishi unaweza fanya kazi nzuri zaidi ya huu upuuzi!jiongeze

    ReplyDelete
  2. Ukiangalia licha yakuwa wakongo wapo vizuri kwenye soka kwenye ukanda wetu huu lakini jauri ya Mazembe kwa kipindi kirefu inajengwa na wachezaji kutoka Zambia hivyo maskauti wa Simba ipohaja ya msingi kabisa ya kuekeza nguvu zao zaidi katika kusajili wachezaji kutoka Zambia. Mimi nnaimani kabisa njia pekee ya Simba kukomesha uteja kwa Tp Mazembe basi ni kwa viongozi wa usajili wa Simba ni kufikiria kuumarisha uti wa mgongo wa timu ya Simba kwa kuimarisha usajili wa wachezaji kadhaa mahiri kutoka Zambia.Nkana,Zesco
    Green warriors,power Dynamo,Mufurira wanderas na kadhalika hizi timu zina utajiri mkubwa wa wachezaji ni jambo la kushangaza kwa timu zetu zinafikia hadi gharama za kumleta mchezaji Tanzania kuja kufanya majaribio kutoka nchi za mbali wakati hata Uganda tu unaweza kupata mchezaji wa kiwango bila ya kuingia gharama.

    ReplyDelete
  3. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic