May 11, 2019



KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa kwa sasa wachezaji wake wamechoka kutokana na kushindwa kupata muda wa kupumzika baada ya kucheza michezo mingi kwa wakati mmoja kwenye ligi.

Akizungumza na Saleh Jembe, Aussems amesema kuwa amecheza michezo 10 ndani ya siku 24 hali ambayo imefanya wachezaji wake wachoke.

"Unajua tumecheza mechi 10 ndani ya siku 24 tu, hili jambo sio jepesi na wachezaji wangu wanachoka wanashindwa kupata muda wa kupumzika, ratiba imewabana wanashindwa kupata muda wa kurejea kwenye ubora wao.

"Bado tuna nafasi ya kufanya vizuri licha ya kupoteza kwenye mechi zetu zote mbili nje na ndani ni jambo la kawaida kwa kuwa huu ni mpira na kitu chochote kinaweza kutokea, mashabiki waendelee kutupa sapoti kuna jambo jema linakuja kwa ajili yao," amesema.

Simba imeshindwa kufurukuta msimu huu mbele ya Kagera Sugar baada ya mchezo wa kwanza uliochezwa Kaitaba kufungwa mabao 2-1 na mchezo wa jana kufungwa bao 1-0.

5 COMMENTS:

  1. Simba ina kawaida ya uzembe fulani hivi linapokuja suala la mechi za viporo angalau mara hii kidogo imejikaza lakini mechi kama hii ya Kagera Dareslaam Yanga hawezi kufanya makosa hata siku moja na kukuali kufungwa kirahisi kama ingeliikuwa wao ndio wapo kwenye viporo. Nashsngaa sana Yanga kuanza kukata tamaa ya ubingwa mapema kwani kwa Simba wanaweza kuzembea wakati wowote na kupoteza mechi zao na kujikuta wakilingana na Yanga kimchezo na kuanza kupigania points za ubingwa.

    ReplyDelete
  2. Kwani kilichowanyima Yanga kushinda ni nini?Hakuna timu nyingine licha ya Simba ambayo ingehimili kucheza mechi 8 ndani ya siku 14.Na kufanikiwa kuongoza ligi.Yanga alipewa nafasi ya kucheza mechi 11 nyumbani tena kwa kupumzika. Wacha visingizio .

    ReplyDelete
  3. kagera hakuna hata mmoja alikuwa na kadi tatu kweli?

    ReplyDelete
  4. Biashara ndio walikuwa nä kadi tatu.Mpaka kocha kapata kiwewe Zahera analalama refa ni mvuta bangi.Simba atachukua ubingwa hamna namna.Shangilieni timu za nje kama kawaida yenu.

    ReplyDelete
  5. Kamwene.Wabaya hawa wamefanya vyura wawe washangiliaji kwa msimu mwingine .

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic