May 17, 2019


KOCHA wa Mbeya City, Ramadhan Nsanzurwimo amesema kuwa kikosi chake kipo tayari kwa mchezo wao wa kesho dhidi ya African Lyon utakaochezwa uwanja wa Uhuru.

Mbeya City leo wamefanya mazoezi yao ya mwisho uwanja wa Uhuru kabla ya kesho kumenyana na Lyon ambayo tayari imeshuka Daraja.

Akizungumza na Saleh Jembe, Nsanzurwimo amesema kwamba wamejipanga kiasi cha kutosha kutafuta ushindi mbele ya Lyon.

"Najua utakuwa mchezo mgumu ila hilo halinipi wasiwasi kwani morali kwa wachezaji ni kubwa nina imani tutapata matokeo, mashabiki wajitokeze kutupa sapoti," amesema.

Mbeya City ipo nafasi ya nane baada ya kucheza michezo 35 imebakiwa na michezo matatu ili kumaliza msimu  huu.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic