May 27, 2019

NAHODHA wa timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta anayekipiga KRC Genk ameweka bayana kwamba yeye sio mfungaji bora kwenye ligi ya Ubelgiji badala yake alikuwa akimpa changamoto mfungaji bora wa msimu uliopita.

Samatta ambaye ametia timu bongo na alipokelewa kwa heshima na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo,Dk. Harrison Mwakyembe, usiku wa kuamkia Jumapili.

"Sina tuzo ya mfungaji bora kwenye Ligi Kuu ya Ubelgiji msimu huu, mfungaji bora ni Hamdi Alboui huyu tulikuwa tunashindana naye ila yeye ametupia mabao 25 mimi nina mabao 23.

"Nafikira mimi ndiye nilikuwa nampa changamoto kwani yeye ndiye alikuwa mfungaji bora msimu uliopita, kwa hiyo nilikuwa najaribu kumvua ubingwa haikuwa bahati," amesema Samatta.

Samatta mkononi mwake ana tuzo ya kiatu cha Mchezaji Bora wa Mwaka Mwenye Asili ya Afrika 'Ebony Shoe'.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic