MLINDA mlango wa timu ya Yanga, Ramadhan Kabwili amesema kuwa amefikia sehemu nzuri ya mazungumzo na uongozi wa timu ya Sudan hivyo anasubiri kwenda muda wowote kuanzia sasa.
Akizungumza na Saleh Jembe, Kabwili amesema kuwa mkataba wake na Yanga unakamilika Mei 30 hivyo bado anaendelea kuangalia ofa zilizopo mezani kabla ya kuondoka Yanga.
"Kweli kwa sasa ndani ya Yanga mkataba wangu unamalizika mwezi huu hivyo nina ofa ambazo zipo mkononi tunaendelea kufanya mazungumzo kabla ya kusaini ambapo ni timu moja ya Sudan ambayo tumefika sehemu nzuri.
"Mazungumzo yakikamilika kila kitu kitakuwa sawa, na nitaiweka wazi timu yenyewe, ila bado sijaikatia tamaa timu yangu ya Yanga kwa kuwa ni sehemu yangu ya kazi na wamenilea pia lazima iwe kipaumbele changu." amesema Kabwili.
0 COMMENTS:
Post a Comment