May 25, 2019


Imeelezwa kuwa klabu ya Simba tayari imempatia nakala ya mkataba mpya kocha mkuu wa klabu hiyo Patrick Aussems ili kuusoma kabla ya kuusaini.

Taarifa imeeleza kuwa mkataba wa awali wa klabu ya Simba na kocha Aussems unaisha mwisho wa msimu huu.

Katika mkataba mpya Simba imeboresha maslahi ya kocha huyo kutoka kulipwa milioni 22.7 hadi milioni 27.5 kwa Mwezi. Pia katika mkataba huo Simba inamtaka kocha huyo kutetea ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara msimu ujao.

Pia kufika hatua ya robo fainali ya klabu bingwa Afrika (CAF Champions League), kuchukua Ubingwa wa Sportpesa Cup na kufanya vizuri kwenye michuano ya Azam Sports Federation Cup na Mapinduzi Cup.

Katika nakala ya mkataba huo Simba inataka kumuongezea kocha Aussems mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mkataba mwingine wa mwaka mmoja zaidi Iwapo atafanya vizuri

Aussems atakuwa kocha anayelipwa mshahara mkubwa zaidi kwa makocha ligi kuu Tanzania Bara anayemfuatia ni kocha msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila anayelipwa mshahara wa milioni 7 kwa mwezi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic