May 25, 2019

LEO Simba itashuka uwanja wa Taifa kucheza mchezo wake wa mwisho wa Ligi Kuu Bara jijini Dar kwa msimu wa mwaka 2018/19 dhidi ya Biashara United.

Mchezo wa kwanza dhidi ya Biashara ulichezwa uwanja wa Karume, Mara ambapo Simba ilishinda kwa jumla ya mabao 2-0.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa mashabiki wa Simba wajitokeze kwa wingi kuona namna watakavyocheza kibingwa na Biashara United.

"Tunacheza kibingwa kwa kuwa tayari tumeshakuwa mabingwa, mashabiki wa Simba njooni kwa wingi uwanja wa Taifa kuona namna mabingwa wanavyocheza na kukabidhiwa kombe" amesema Manara.

Mchezo wa mwisho kwa Simba itacheza dhidi ya Mtibwa Sugar Mei 28 uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic