Ngassa aliugua ghafla jana wakati timu yake ikijiandaa kuivaa Ruvu Shooting mchezo uliochezwa uwanja wa Uhuru hakuwa sehemu ya kikosi kutokana na kuondolewa na daktari wa timu hiyo Edward Bavu.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ngassa amesema kuwa anamshukuru Mungu kwa kuwa kwa sasa anaendelea vizuri hivyo muda wowote atarejea uwanjani.
"Nilikuwa nasumbuliwa na Malaria, ila kwa sasa nipo fiti naendelea vizuri, nina imani baada ya muda nitarejea kwenye kikosi kuendelea kupambana," amesema Ngassa.
0 COMMENTS:
Post a Comment