May 15, 2019


WINGA machachari wa KMC, Hassan Kabunda amesema kuwa ushindi wao wa kwanza ugenini umetokana na hasira walizonazo za kutimiza malengo ambayo wamejiwekea kabla ya kumaliza msimu.

KMC ambayo imepanda Daraja msimu huu, kwenye michezo 10 ambayo wamecheza ugenini hawakufanikiwa kuambulia pointi tatu, bali waliishia kupata sare na vipigo hivyo ushindi wao mbele ya Tanzania Prisons uwanja wa Sokoine ulikuwa ni wa kwanza kwao.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kabunda amesema kuwa wamepanga kumaliza ligi wakiwa kwenye nafasi nne za juu hivyo lengo lao haliwezi kutimia bila kupata pointi tatu.

"Tuna kazi ngumu ya kufikia malengo yetu ambayo ni kuona timu yetu inamaliza ikiwa nafasi ya nne, hivyo hilo halitatimia kama hatutashinda michezo yetu, ushindi wetu wa kwanza ugenini kwetu ni furaha," amesema Kabunda.

KMC ipo nafasi ya nne baada ya kucheza michezo 36 imebakiwa na michezo miwili ili kumaliza msimu huu wa 2018/19.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic