May 15, 2019

UONGOZI wa Azam FC umewataka mashabiki na viongozi wa Simba kuacha maneno ambayo yanadaiwa kwa sasa kwamba wameibania Simba baada ya kutoka nao sare kwenye mchezo wao wa juzi uliochezwa uwanja wa Uhuru.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema kuwa amekua akisikia maneno kutoka kwa mashabiki na viongozi wa Simba wakilalamika kwamba Azam wameibania Simba kutangazwa kuwa mabingwa.

"Baada ya sare yetu na Simba tuliyoipata uwanja wa Uhuru, mashabiki na viongozi wa Simba wamesikika wakilalamika kwamba tumewabania kuwapa ubingwa, niseme tu kwamba Azam ni timu kubwa na inapambana kupata matokeo bila kujali inacheza na nani.

"Kumekuwa na kasumba kwamba kama tukiwafunga wakongwe wa ligi ambao ni Simba na Yanga inadaiwa tumewabania hata tukitoka nao sare wanasema tumewabania, sisi hatupo kwenye ligi kwa ajili ya kumnufaisha mtu, tupo kwenye ligi kwa maslahi ya kampuni yetu ya Azam FC.

"Kushinda, kushindwa na kupoteza ni sehemu ya matokeo na anayeamua matokeo ni kocha kwa namna atakavyoingia na mbinu zake, tulipoteza mchezo wetu wa kwanza mbele ya Simba tukakubali, tukajipanga kupata ushindi tumeambulia sare, sasa kwa nini walalamike, huu ni mpira," amesema Maganga.

Kocha wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa wachezaji wake walipambana kupata matokeo ila bahati haikuwa yao kutokana na uchovu.

"Mchezo wetu dhidi ya Azam FC haukuwa mwepesi, ulikuwa ni mchezo mgumu na tulipambana kupata matokeo bahati haikuwa kwetu.

"Wachezaji wangu walitengeneza nafasi ila walishindwa kuzitumia hivyo nina imani wakati ujao tutafanya vizuri," amesema Aussems.

5 COMMENTS:

  1. Kwani uongo mlikaza na kuibania Simba lkn mkicheza na Yanga hamkazi na kama unabisha fanya marejesho kwenye Azam TV.Hata mkaze vipi ubingwa Simba anauchukua na mje kuendelea kushangilia timu za kigeni.

    ReplyDelete
  2. Jamaa wamezoea Kubebwa !!
    japo wamiliki wa Azam ni wapenzi wa lakini isiwe sababu ya kuwaachia tumieni jasho lenu acheni mambo ya mbeleko

    ReplyDelete
  3. Huu upuuzi siupendi Simba tucheze mpira na Kila mechi tupate ushindi yusicheze mpira kwa mdomo.

    ReplyDelete
  4. sioni mantiki kwenye bango hili Maganga

    ReplyDelete
  5. Mimi ni Simba lakini sipendi kuachiwa eti Azam atuachie mechi tushinde , hapana. Simba ipambane tuwafunge na uwezo huo tunao na mpira simba ilicheza vizuri tulitakiwa kuongeza mbinu na nguvu tupate ushindi. Hata hivyo sare ni sehemu ya mchezo, bado Simba tuna nguvu na uwezo wa kushinda mechi zet zilizobaki na kwa bingwa. Muhimu wachezaji kutobweteka. Chezeni kwa nguvu zote na maue MAGOLI ndio USHINDI acheni chenga nyingi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic