May 10, 2019



Kamati ya waandaji wa Ndondo Cup wakishirikiana na chama cha mpira cha Dar es salaam (DRFA) wamekabidhiwa mipira 50 ambayo leo itaanza kutumika katika ufunguzi wa michuano hayo.

Hii ni mipira 20 kati ya 50 imekabidhiwa katika ofisi za vyama  vitano vya mpira wa miguu vya wilaya zote za mkoa wa Dar.

Mashindano ya Ndondo Cup yalitakiwa kuanza kutimua vumbi Mei 3 ila yaliahirishwa na kusogezwa mbele ili kuupisha msiba wa ndugu Reginald Mengi.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza leo Ijumaa  kwa kuzikutanisha timu za Mabibo Combine na Misewe Boys katika Uwanja wa Kinesi,Shekilango Jijini Dar.

Mwenyekiti wa chama cha mkoa  wa Dar es Salaam, Almas Kasongo amesema ni hatua kubwa sana kutumia mipira kutoka CAF kutumika Ndondo Cup.

"Ndondo Cup sasa ni wazi inatambulika na CAF ndio maana tunatumia mipira yao hivyo naamini ndondo cup hii itatoa vipaji vingi sana," amesema Kasongo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic