May 10, 2019



Si ukisema rekodi imeandikwa katika mchezo wa soka barani Ulaya.

Timu kutoka Ligi Kuu England maarufu kama EPL ndio zilizoandika rekodi hiyo baada ya kubeba makombe yote mawili makubwa ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Europa League hata kabla ya kucheza fainali.


Ligi ya Mabingwa; fainali ni kati ya Liverpool dhidi ya Tottenham na Europa League ni Chelsea dhidi ya Arsenal, timu zote nne zinatokea katika Ligi Kuu England.


Hii sasa inaweza kuwa njia lahisi kusema kweli EPL ndio ligi bora ya soka duniani kote.


Kabla ligi hiyo imekuwa ikipata upinzani mkubwa kujinadi ni bora raidi kwa kuwa timu zake zimekuwa hazifanyi vizuri kwenye michuano hiyo miwili maarufu chini ya Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) na kuiacha Hispania ikitamba zaidi.


2 COMMENTS:

  1. Bora wap mbona mara kibao yote mawili(2)yameenda hispain na hausemagi laliga league bora ..huo ni uongo..

    ReplyDelete
    Replies
    1. kuwa mwelewa kidogo basi umeambiwa kabla fainali hazijapigwa makombe yote yanauhakika wa kutua england,haya sema wewe lini spain waliingiza timu nne katika fainali?yaani kwa maana hiyo england washabeba makombe matatu mpaka sasa uefa,europa,super cup

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic