May 9, 2019


Ni kama mambo yameiva vile juu ya Yanga na kipa Beno Kakolanya ambapo taarifa zilizopo zinaeleza kuwa uongozi wa klabu yake umeamua kuachana naye rasmi.

Taarifa zinasema kuwa baada ya uongozi mpya kuingia madarakani chini ya Mwenyekiti wake Mshindo Msolla, umeamua kuketi chini na kufikia mwafaka wa kuachana na Kakolanya.

Ikimbukwe Kakolanya akiingia kwenye sintofahamu na Kocha wake Mwinyi Zahera mpaka kufikia hatua ya kumtema kikosini na mpaka sasa akawa hana timu ya kuchezea.

Kakolanya aligoma kuendelea na kazi Yanga kutokana na kutolipwa fedha zake za mshahara pamoja na za usajili hivyo kuamua kujiondoa mwenyewe kwa kuanza kugomea mechi.

Kuondoka kwa Kakolanya Yanga kunamfanya sasa awe huru na timu yoyote inaweza kumsajili hivi sasa.

3 COMMENTS:

  1. jiokoteen embe dodo hilo bangusilo

    ReplyDelete
  2. SIMBA MPO WAPI KIJANA HUYU SAFI SANA GOLINI TUMCHUKUE FASTA

    ReplyDelete
  3. Simba nakuusieni kidume msikiache hicho japo Kwanza Kwa mkataba WA mwaka mmoja na Fei Toto mwenye mkataba WA mwaka mmoja Pia msimuache. Yule wa Kenya mshanbulizi mwenza WA Kagere msimuache watakuja kuokotwa na wengine mlie mje mjute. Kwani mmessahau jinsi yanga walivokufanyeni pale mlipokuwa wanyonge walikunyanganyeni Yule beki Mrundi kavukavu bila ya hata uungwana WA kukulipeni zile hela mlizomtangulizia Yule mchezaji. Leo hii ingelikuwa hawa jamaa wangelikuwa na uwezo ule WA Manji wasingebakia na Kagere, Boko wala Okwi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic