May 22, 2019








Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeingia mkataba ushirikiano wa miaka mitatu ya Laliga.


Kauli hiyo ilitolewa na Rais wa TFF, Wallace Karia katika mkutano wa Waandishi wa Habari uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


TFF juzi imepokea ugeni wa klabu ya Sevilla ya nchini Hispania ulioratibiwa na Kampuni ya SportPesa, Laliga na TFF.



Akizungumza na Waandishi wa Habari, Karia alitoa shukrani kwa SportPesa kwa kufanikisha ujio wa Sevilla ambao anaamini utakuwa na maganikio kwa  TFF na kwa wachezaji wa Simba.


Karia alisema, makubaliano waliyafikia hivi karibuni na Laliga na kikubwa katika kuleta ushirikiano wa kisoka ili kufikia levo za kimataifa.


Aliongeza kuwa, kwa kupitia ujio wa Sevilla klabu zao zitapata mafanikio kutokana na kliniki waliyowapa viongozi wa klabu leo (Jana).


"Pongezi nyingi zihende kwa SportPesa ambao wao wamekuwa wadau wetu wazuri katika kukuza na kuendeleza Soka nchini.



" Hivyo ushirikiano huo wa Laliga tulioupata TFF ni daraja la mafanikio kwetu katika kukuza na kuendeleza soka nchini,"alisema Karia

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic