May 22, 2019



Simba wanajiamini wataocheza soka la kuvutia kiasi kwamba Sevilla nao wataona shida kukutana na Msimbazi.


Timu hizo zinakutana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kesho katika mechi ya kirafiki ya kimataifa iliyoandaliwa na SportPesa.

Kocha Mkuu wa Simba Mbelgiji, Patrick Aussem ameahidi kuwatandazia soka safi wapinzani wao Sevilla ya Hispania.

Simba wataingia uwanjani hapo wakiwa tayari wametangazwa kuwa Mabingwa wapya wa Ligi Kuu Bara baada ya juzi kuwafunga Singida United na kujihakikishia ubingwa huo.

Akizungumza na Mwandishi wa Habari kwa niaba ya kocha huyo, Afisa Mtendaji Mkuu (C.E.O) wa Kumpuni ya Klabu ya Simba, Cresecentius Magori alisema kuwa juzi usiku alikutana na kocha huyo baada ya mchezo wa Singida na kuzungumza naye katika kuelekea mchezo huo.
Magori katika mazungumzo hayo, Kocha huyo ameahidi kupanga kikosi imara cha ushindi huku wakionyesha kiwango kikubwa.


Aliongeza kuwa, anataka kupata ushindi katika mchezo kwa lengo la kuchukua kikombe kikichowekwa ili waweke rekodi ya kuchukua kikombe cha pili mfululizo baada kile cha ligi.


"Tunafahamu umuhimu mkubwa wa mchezo huu wa kirafiki wa kimataifa, hivyo ni lazima tushinde ili tuweke historia.


"Aliniahidi hayo mara baada ya mchezo wa ligi na Singida ambao tuliwafunga mabao 2-0 na kutangaza ubingwa huo wa ligi.

"Hivyo, Kocha wetu ameniahidi hilo kikubwa mashabiki wanatakiwa kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo kwa ajili ya kuisapoti timu yao,"alisema Magori.


Naye Rais wa Sevilla, Jose Ramon Carmona alisema kuwa "Nianze kwa kuishukuru SportPesa kwa kufanikisha ujio wetu kwa kuwa klabu ya kwanza Laliga kufika hapa nchini Tanzania.


"Kuhusu maandalizi yapo vizuri ya mchezo huu, tumepata taarifa za Simba kuchukua ubingwa wa 20 jana (juzi), hivyo niwapongeze kwa hilo, hivyo tutaingia uwanjani kwa ajili ya kazi moja pekee ya ushindi.

1 COMMENTS:

  1. Mmmmh biv hii blogu ndo imekosa watu makin kias hiki Simba na Singida si wamecheza jana halaf habar inasema et Simba wamekuwa mabingwa baada ya juz kumfunga Singida.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic