May 22, 2019

UONGOZI wa Azam FC, umesema kuwa kwa sasa hauna mpango wa kumsajili kiungo wa Yanga, Feisal Salum kwa kuwa bado ni mali ya Yanga na kocha hajapendekeza majina ya wachezaji wanaohitajika.

Fei Toto amekuwa akihusishwa kujiunga na Azam FC msimu ujao kutokana na uwezo ambao ameuonyesha msimu huu pamoja na timu nyingine nje ya Afrika.

Akizungumza na Saleh Jembe, mratibu wa Azam FC, Philip Alando amesema bado hawajaanza michakato ya usajili mipya.

"Dirisha la usajili bado halijafunguliwa na hatujafanya mazungumzo yoyote na Fei Toto, kikubwa ambacho Azam FC tunasimamia ni kuona namna gani wachezaji wetu ndani ya timu tunawaongezea mikataba pamoja ili kuboresha kikosi chetu.

"Dirisha la usajili halijafunguliwa na hakuna mchezaji ambaye tumeanza naye mazungumzo, Fei ni mchezaji mzuri hivyo atabaki kuwa mali ya Yanga," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic