May 10, 2019


LEO Ligi Kuu Bara inaendelea leo ambapo timu nne zinatarajiwa kushuka uwanjani majira yaa saa 10:00 kumenyana kwenye viwanja viwili tofauti.

Simba itakuwa nyumbani Dar, uwanja wa Uhuru ikimenyana na Kagera Sugar majira ya saa 10:00.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Kaitaba Simba ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 hivyo leo utakuwa ni mchezo wa kisasi.

Biashara United itaikaribisha Yanga uwanja wa Karume majira ya saa 10:00.

Mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Taifa, Biashara United ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 nao pia leo watakuwa na hasira za kufungwa mchezo wao wa kwanza

1 COMMENTS:

  1. Haya Biashara ipo nyumbani na Simba wapo nyumbani. Dk. 90 ndiyo msema kweli

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic