May 13, 2019


Wakati Yanga ikijipanga kukisuka upya kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao, wadau mbalimbali wamependekeza kutafutwa kwa Kocha Msaidizi ambaye atamsaidia Zahera

Inafahamika Kocha Noel Mwandila aliletwa nchini na George Lwandamina aliyekuwa kocha wa Yanga msimu uliopita na jukumu lake lilikuwa kuwa kocha wa viungo

Hata hivyo baada ya kuondolewa Shedrack Nsajigwa, Yanga haikupata mbadala wake hivyo Mwandila kulazimika kushika majukumu hayo

Wengi wanaamini ni vyema Yanga ikapata kocha Msaidizi mzawa ambaye anawafahamu vizuri wachezaji wa Kitanzania na mwenye kuzijua 'fitna'za soka letu ili Mwandila abaki na majukumu yake aliyosomea

Katibu Mkuu wa zamani wa Yanga Charles Mkwasa aliwahi kutangaza mchakato wa kutafutwa kocha Msaidizi.

Hata hivyo mchakato huo haukukamilika baada ya Mkwasa kuugua na kulazimika kuacha majukumu ya uongozi kutokana na maradhi ya moyo yaliyosababisha apelekwe India kutibiwa

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic