May 10, 2019

HISTORIA mpya imeandikwa kwa klabu ya Yanga ambayo baada ya kupata viongozi wapya ambao wataiongoza timu yao.

Mchakato mzima ulivyokwenda kwa haki na uwazi bila bugudha yoyote ile kwa hilo mlilofanya wanachama wa Yanga pamoja na mashabiki mnastahili pongezi.

Awali niliwaambia kwamba mnapaswa mfanye uchaguzi kwa kutazama sera baada ya kuzisoma na kuzielewa na sio kwa mgongo wa fedha hilo lingewaumbua baadaye.

Nimeona na nimefuatilia mchakato mzima ulivyokwenda, sera makini na viongozi makini wote wameonyesha ukomavu wao na kukubali matokeo.

Huo ni ukomavu wa kishujaa na upendo ambao unapaswa uwepo siku zote na sio baada ya uchaguzi tunarejea kwenye makundi tena sio sawa.

Kikubwa ambacho napenda kutoa rai kwa walioshindwa ni kukubali matokeo na kusonga mbele hakuna haja ya kujikatia tamaa maisha lazima yaendelee.

Kwa walioshinda sasa mtihani wao ndo unaanza kuwa mkubwa tofauti na vie ambavyo walitarajia kwamba mambo yatakuwa mteremko hakuna kitu kama hicho.

Kama ambavyo uchaguzi ulikuwa wa haki basi nao wanapaswa watende haki katika kila mambo ambayo watayafanya kuanzia sasa mpaka muda wao utakapoisha.

Mchezo wa kujiuzulu baada ya kuboronga uwe ni wimbo ambao hautapewa nafasi bali utendaji bora uwe ni kipaumbele cha kwanza kwa kila kiongozi.

Narudia sasa kuwapa hongera Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kufanikiwa kurejea upya kwa wanachama kisha mambo kwenda sawa awali walitaka kwenda namna ambavyo wanataka matokeo yakawa magumu kupatikana.

Wanachama kama hawajakuelewa inabidi uwaeleweshe ili mambo yaende na sio utumie nguvu zako kwa kuwa wewe ni mkubwa hapana demokrasia inaiongoza nchi yetu.

Kwa hatua mliyofikia pia mnapaswa hongera kwa kuwa mlikuwa waelewa na mkajua wanachama wanataka nini na matokeo yake mkapata kilicho bora, lengo ni moja kuwa na timu bora.

Ninaamini wanachama ambao walijitoa kuchagua walikuwa wana mawazo yao, kwenye vichwa  vyao kwa sasa ni kuona sasa kunakuwa na mabadiliko ndani ya timu.

Mabadiliko hayo yaanaanzia kwenye kikosi bora ambacho kitakuwa kinawapa burudani na vicheko wakiwa wanapita mitaani kwa majirani zao huku wakitamba kuhusu umuhimu wa kura yao.

Wanachama wanahitaji matokeo chanya katika masuala yote, uongozi hasa utendaji na matokeo chanya uwanjani kwa timu hilo ndilo deni la viongozi wote mliochaguliwa.

Mna kazi ya kuwafanya watembee vifua mbele kutokana na matokeo ambayo mmeyapata, wamewaamini na kuwapa nafasi ni muda wenu kutenda kwa vitendo.

Nakumbuka kuna ahadi ya mgombea mmoja ngazi za juu alisema kuwa akichaguliwa wanachama watachoka kunyanyua makwapa kushangilia vikombe, hilo ndilo ambalo linatakiwa sasa liwekwe kwenye mpango kazi.

Vikombe ambavyo wanachama wanahitaji ni hatua ya ndani na kimataifa, hili ni jambo la muhimu kwa kuwa hakuna ambaye hajaona Yanga ikibeba mara nyingi ligi ya ndani sasa inabidi iwe zamu ya kimataifa.

Kila kitu kinawezekana kama mmechaguliwa na kupewa timu hapo ndipo mnatakiwa muanze kwa kutengeneza timu bora na yenye nguvu na sera ya Yanga inasema daima mbele nyuma mwiko.

Pia maboresho ya viwanja kwa wakatika isipuuzwe, ilivyokuwa kwenye sera zenu na itimizwe kwa wakati, ifike wakati Yanga iwe inafanya mazoezi kwenye uwanja wao wa nyumbani sio kila siku wanakuwa wageni.

Jengo la Yanga pia si sehemu ya kuacha, maboresho ya miundombinu ni kitu cha muhimu na kiliimbwa sana kwenye kampeni basi nyimbo zote zilizoimbwa muda wa kucheza ndo sasa.

Mashabiki msiwaache viongozi wawe peke yao shirikianeni katika kila jambo kuona namna gani mnapata matokeo chanya kwa vile ambavyo mnahitaji kuvipata.

2 COMMENTS:

  1. Mashallah covering ya uchaguzi ni kubwa Sana sijaiona Kwa timu nyengine
    yoyte

    ReplyDelete
  2. Wazee wa Yanga mkutane mapema msome dua ama sivyo hali ya timu kwa mechi zilizobakia itazidi kuwa mbaya...virusi visomewe dua viondoke nyota ya ushindi irudi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic