YANGA HII USIPIME!! MSOLLA AANZA NA WINGA HATARI MBEYA CITY
MUDA wowote Yanga ya Mshindo Msolla huenda wakamalizana na winga wa Mbeya City, Iddi Selemani kwani anawasikilizia wao tu.
Zahera anavutiwa na kiwango cha nyota huyo ambaye aliwafunga bao moja kwenye Ligi na baadaye alifanya hivyo kwenye mchezo wao na Simba pia.
Iddi Selemani alisema; “Ni kweli nilishazungumza na kocha wa Yanga, ila kuna hata wachezaji wenzangu wengi amezungumza nao, hivyo kama kweli ana nia ya kutusajili basi tutajua tu baada ya ligi kumalizika, kama walivyoniahidi.”
“Kwa upande wangu hadi sasa sina mkataba na Mbeya City hivyo naangalia zaidi masilahi yangu kwa sasa,” alisema Selemani.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe alisema: Ofa wala mazungumzo ya Yanga na Iddi sisi hayajatufikia, hivyo kama mambo yatakuwepo basi itajulikana mbeleni.”
“Ila wanachotakiwa wao kukijua zaidi ni kwamba, hata sisi bado tuko na mipango na Iddi ya kuendelea kumtumia maana ni mchezaji bora kwetu hivyo suala hilo litategemea zaidi muda halisi wa usajili ukifika.
0 COMMENTS:
Post a Comment