OFISA Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa leo wamejipanga kuwapapasa wapinzani wao Yanga, uwanja wa Uhuru hivyo wajiandae kisaikolojia.
Bwire amesema kwa sasa wameanza ligi upya hivyo ni lazima wawanyooshe vigogo hao kwa namna yoyote ile ili wabebe pointi tatu.
"Tumewapapasa wababe wao Lipuli, sasa hapo unadhani kwao nini kitatokea? Hamna namna lazima wapapaswe tu maana kwa sasa sera yetu ya Papasa Square inaendelea hivyo wajipange kwelikweli," amesema Bwire.
Ruvu Shooting ipo nafasi ya 14 baada ya kucheza michezo 35 imejikusanyia pointi 42 na imebakiwa na michezo mitatu kukamilisha mzunguko wa pili msimu huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment