May 13, 2019


MSHAMBULIAJI wa timu ya Yanga, Amiss Tambwe amesema kuwa kikosi cha Yanga ni imara na kinauwezo wa kushindana na timu yoyote ndani na nje ya Tanzania kama ilivyo Simba.

Tambwe ambaye amecheza timu zote mbili kubwa za bongo, ambao ni Simba na Yanga mpaka sasa amepachika mabao 72 kwenye Ligi Kuu Bara baada ya kutua bongo.

"Yanga ni timu imara na ina uwezo wa kushindana na timu nyingi hapa bongo na nje ya bongo, kwa kuwa tumecheza mechi nyingi za kimataifa hali inayotufanya tuwe imara kwenye ushindani.

"Kwa sasa ni suala la mpito tu ambalo tunalipitia ila bado wachezaji tunafanya vizuri hata ukitazama mpaka sasa tumepambana na tumejikusanyia pointi 80 kwenye ligi si haba, hata wapinzani wetu Simba nao wapo vizuri isipokuwa tunapishana vitu vidogo tu na ndio maana tunashindana nao," amesema Tambwe.

3 COMMENTS:

  1. Kwani huyo Tambwe ai yumo katika list ya kutemwa au ndio jaribio la kubakia?

    ReplyDelete
  2. Ni kick za kubakia

    ReplyDelete
  3. Huyu Kocha ndio maana anatakiwa asimamiwe na asiwafanye Yanga wote ni wajinga haiwezekani atamke kuwa eti atasajili wachezaji 8 tu....hata asiye na akili na soka anaelewa kuwa Yanga imekuwa dhaifu mno na zaidi ya 3/4 ya wachezaji waliopo kikosini hawafai hata kuendelea kubaki Yanga....sasa atakujaje na kusema atasajili wachezaji 8 tu? Ndio maana wanayanga wanahamasishwa kuchangia na kukusanya fedha ili waunde timu imara na kusajili wachezaji bora wa kutosha waondokane na hali iliyopo...tatizo halitakuwa pesa tena kwani watakuwa na fedha ya kutosha kusajili na kulipa mishahara....asiwafanye wanayanga warudi kule walipotoka kwa kuwa na kikosi dhaifu chenye wachezaji wa nje na ndani ya nchi ambao wengi wao ni magarasa wa kiwango cha chini ambao hata wakicheza na Lipuli, Ndanda, Singida United wanafikiria "kupaki basi". Yanga wanataka wachezaji wa kiwango cha juu mno wakushindana na kutoa upinzani wa hali ya buy kwa timu kama Simba, TP Mazembe, Al Ahly nk...hata kama hawata shiriki mashindano ya CAF lakini wataisaidia kuchukua ubingwa wa ligi hayo ndio matamanio na mahitaji yao wapenzi na wakereketwa wa Yanga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic