May 13, 2019


IMEELEZWA kuwa nyota 10 wa kikosi cha kwanza wakiongozwa na nahodha, John Bocco ndani ya Simba mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu hivyo panga la kuwakata amekabidhiwa Kocha Mkuu, Patrick Aussems.

Habari kutoka ndani zimeeleza kuwa Simba haina mpango wa kumuacha staa hata mmoja kutokana na umuhimu wa wachezaji hao hivyo wanasubiri ripoti kutoka kwa kocha mkuu ndiyo itakayoamua.

"Suala la kuwaacha wachezaji ndani ya Simba na nani tunamhitaji hilo lipo mikononi mwa kocha hivyo yeye akisema sisi tunafanya," ilieleza taarifa hiyo.

Wachezaji hao ambao mikataba yao ipo ukingoni ni pamoja na :- Asante Kwasi, Nicholas Gyan, ambao ni raia wa Ghana, Haruna Niyonzima wa Rwanda, Emmanuel Okwi wa Uganda, Juuko Murshid wa Uganda, John Bocco, Erasto Nyoni, Aishi Manula, Shomari Kapombe na Salum Mbonde ambaye tayari ameshatemwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic