May 13, 2019


MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema wachezaji wake wanastahii pongezi kwa kuwa wamepambana mwanzo mwisho kwa ajili ya kutafuta matokeo.

Liverpool, wamemaliza ligi msimu huu wakiwa nafasi ya pili wakiwa na pointi 97 wamepishana pointi moja na mpinzani wake Manchester City ambaye ametwaa kombe jana baada ya kufikisha pointi 98.

"Tumemaliza vizuri ni jambo la kushukuru kwa hatua ambayo tumefikia, kila mmoja alipambana kwa ajili ya timu na ameweza kufanya kile ambacho amekifanya na matokeo yake tupo hapa tulipo sasa," amesema Klopp.

Liverpool katika michezo 38 ambayo wamecheza wamepoteza mchezo mmoja pekee huku wakishinda michezo 30 na wametoa sare saba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic