May 10, 2019


Mbali na Simba kupoteza 1-0 Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, watani zao wa jadi Yanga waliokuwa Karume Stadium huko Musoma mkoani Mara wameshindwa kutamba mbele ya Biashara United kwa kupoteza bao 1-0.

Bao pekee la mchezo huo limewekwa kimiani na mshambuliaji Tariq Seif kunako dakika ya tisa tu ya mchezo baada ya mabeki wa Yanga kumuacha mchezaji huyo peke yake wakidhani ameotea.

Ushindi wa Biashara unawafanya wafikishe alama 40 kutoka 37 ambazo walikuwa nazo kabla ya mechi ya leo.

Yanga nao wanazidi kusalia na alama zao 80 wakiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi na wakiwa wamecheza jumla ya mechi 35.

3 COMMENTS:

  1. Itakuwa hawa biashara leo wamependelewa!

    ReplyDelete
  2. Kuna tatizo pale Yanga hasa inapoenda kucheza mikoani...

    ReplyDelete
  3. Wazee wa Yanga mkutane mapema msome dua ama sivyo hali ya timu kwa mechi zilizobakia itazidi kuwa mbaya...virusi visomewe dua viondoke nyota ya ushindi irudi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic