May 10, 2019


Dakika 90 zimemalizika katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kwa Simba kuendelea kuwa kibonde wa Kagera Sugar baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0.

Bao pekee la mchezo huo limepatikana mnamo dakika ya 42 kipindi cha kwanza kwa Mohammed Hussein kujifunga ikiwa ni baada ya kukosa mawasiliano mazuri baina yake na kipa Aishi Manula kufuatia mpira uliopigwa na mchezaji wa Kagera.

Licha ya kutawala sehemu kubwa ya mchezo, Kagera Sugar walionekana kulinda kwa umakini zaidi lango haswa baada ya kupata bao la kuongoza na kuwafanya Simba kushindwa kucheka na nyavu zao.

Kunako kipindi cha pili cha mchezo, Kocha wa Simba Patrick Aussems aliwafanyia mabadiliko wachezaji Hassan Dilunga aliyemtoa na nafasi yake kuchukuliwa na Rashid Juma huku James Kotei naye akitolewa na Jonas Mkude akichukua nafasi yake.

Mabadiliko hayaikuisaidia chochote Simba ambapo mpaka dakika 90 zinamalizika matokeo yalisalia kuwa 1-0.

Kuendelea kupoteza kwa Simba dhidi ya Kagera kunawafanya wazidi kusalia nafasi ya kwanza wakiwa na alama zao 81 kwenye nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi huku Kagera wakijiongezea alama tatu muhimu wakifikisha alama 43.


4 COMMENTS:

  1. Itakuwa hawa Simba leo hawajapendelewa!

    ReplyDelete
  2. Duh....timu ileile inaendelea kutusumbua swali ni kwanini? Ni kweli mchezo wa soka una matokeo matatu (kushinda, sare na kufungwa) lakini haiwezekani timu moja iwafunge mara 3 mfululizo ndani ya michezo 4

    ReplyDelete
  3. Simba wamechoka mechi 7 siku 14!
    Na kuna bahati kwenye mpira kama Yanga walivyopata bahati msimu ws kwanza wa ligi!Hata Zahera alikiri alikuwa anajua wao ni wa 6 au 7...lakini kwa bahati wakawa wanashinda tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic