May 14, 2019


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mkongomani, Mwinyi Zahera amesema kamwe hatanyamaza kulikosoa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) pale makosa yanapofanyika.

Mkongomani huyo alitoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache tangu apokee barua ya mashitaka kutoka Bodi ya Ligi Kuu Bara akitakiwa kujieleza juu ya tuhuma mbalimbali anazotoa kutokana na uendeshaji wa ligi.

Zahera hivi karibuni aliwavaa waamuzi waliochezesha mchezo wa Yanga dhidi ya Biashara United kwa kukubali bao ambalo mfungaji alikuwa ameotea kwenye Uwanja wa Karume, Musoma.

“Bodi ya ligi walinitumia barua wakitaka nikajieleze. Lakini nimesema sitaacha kuzungumza pale ninapoona timu yangu haitendewi haki.

“Hembu angalia lile bao walilotufunga Biashara lilikuwa sahihi? Hii ni aibu, kwa mtindo huu soka la Tanzania haliwezi kuendelea,” alisema Zahera.

Zahera ni kati ya makocha wanne wa timu zinazoshiriki ligi kuu walioitwa kujieleza Kamati ya Nidhamu ya TFF kutokana na tuhuma mbalimbali walizotoa.

Wengine ni Athuman Bilal wa Stand United, Nassoro Mrisho (Geita Gold FC) na Ramadhani Nsanzurwimo (Mbeya City).

1 COMMENTS:

  1. This is too much....kila siku kelele....hivi hakuna mtu mwenye ustaarabu hapo Yanga wa kumwambia aache malalamiko mengi akazanie kukisuka kikosi chake??? Its shameful as professional coach to act this way over and over!!!!its despicable and detestable to always hear all of these foolishness from the same person!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic