YANGA YA MSIMU UJAO NI KAA MBALI NA WATOTO, STRAIKA MWINGINE AONGEZWA
RASMI Klabu ya Singida United, kupitia kwa mkurugenzi wake Festo Sanga, imesema ipo tayari kumuachia kiungo wao Kenny Ally atue Jangwani kama alivyoahidi mmiliki wa timu hiyo, Mwigulu Nchemba.
Kenny ambaye alijiunga na Singida United akitokea Mbeya City misimu miwili iliyopita, mara kadhaa amekuwa akiwindwa na Yanga lakini uongozi wa Singida uligoma kumuachia huru kufuatia kuwa na mchango mkubwa kwenye safu ya kiungo chao.
Sanga alisema kuwa, hawana kipingamizi tena na suala la kumruhusu kiungo huyo, zaidi wanasubiri ligi iishe kisha aende kujiunga na Yanga kama mwenyekiti wao alivyotaka kuwasaidia ingawa hata wao walihitaji sana huduma yake.
“Kutokana na ombi hilo la Yanga, tayari tumeshamruhusu Kenny Ally kufanya maamuzi yake, hivyo akipenda kwenda sisi hatuna kipingamizi kwani tayari tumeshaanza kusajili wachezaji wapya watakaokuja kuziba mapengo yote msimu ujao.
“Tuna wachezaji zaidi ya watatu ambao tumeshamalizana nao katika klabu za Zanzibar, sema siwezi kuwaanika hadi ligi itakapomalizika ndiyo nitaanza kuwatambulisha na watu wataijua tu nia yetu ya kuboresha kikosi msimu ujao,” alisema Sanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment