June 11, 2019

MLINDA mlango wa Simba, Aishi Manula ameongeza mkataba wa miaka mitatu kuendelea kuitumikia klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Kariakoo, Msimbazi.

Manula anakuwa mchezaji wa pili kutambulishwa rasmi kuongeza mkataba ndani ya klabu hiyo baada ya jana mchezaji John Bocco kutangazwa rasmi kwamba ameshamalizana na klabu hiyo kwa kuongeza mkataba wa maika miwili.

Kwa sasa Manula yupo nchini Misri akiwa na timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' ambayo imeweka kambi kwa ajili ya michuano ya Afcon inayotarajiwa kuanza Juni 21.

1 COMMENTS:

  1. Ni utaratibu mzuri kuwapa mkataba wenye umri huu haswa wachezaji tegemeo kikosini, ni vema na itapendeza zaidi pia mkataba ya aina hii wapatiwe pia Tshabalala, Mkude, Nyoni, Kapombe n.k.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic