June 12, 2019


Imeelezwa kuwa Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amewashangaa viongozi ya klabu hiyo kwa kuanza majadiliano ya kumpa mkataba mpya nahodha wa timu hiyo Ibrahim Ajibu.

Taarifa imeeleza kuwa Zahera amesema tangu Ajibu akatae kujiunga na TP Mazembe yeye alishamuondoa kwenye mipango yake ya msimu ujao.

Zahera ambaye kwa sasa yuko Hispania katika majukumu ya timu ya Taifa ya DR Congo inayojiandaa na fainali za AFCON 2019, ameshangaa sana kuona uongozi wa Yanga umeanza kumbembeleza nyota huyo asaini mkataba mpya.

Zahera ameenda mbali na kusema ripoti yake aliyokabidhi kwa uongozi haina jina la Ajibu na anashangaa viongozi wanamtaka Ajibu yupi wakati ameshamuondoa kwenye mipango yake.

Kwa sasa Zahera yuko Misri na kikosi cha timu ya Taifa ya Congo kwa ajili ya michuano ya AFCON inayotaraji kuanza hivi karibuni.

4 COMMENTS:

  1. Ajibu kapigwa chini Hahaaaa. Masikini Ajib Zahera anasema hamtaki

    ReplyDelete
    Replies
    1. We ndio hujui kinacho endelea. Ajibu tayari alisha mwaga wino Simba sc, atasajiliwa vipi na Yanga?

      Delete
  2. Ndipo nawe ndugu yangu kwakunijulisha hayo

    ReplyDelete
  3. Nani wakumpiga chini na huyo tayari kesharejea kwao hamuoni anavopiga chenga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic