ALIYETAJWA KUTUA SIMBA AMALIZANA NA YANGA KWA MIAKA MIWILI
Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza kuingia mkataba wa miaka na straika aliyekuwa anaicheza Polisi ya Uganda, Juma Balinya,
Balinya amekuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Uganda kwa msimu uliomalizika hivi karibuni.
Ikumbukwe awali Balinya alitajwa kuhitajika Simba lakini kilichotokea imekuwa tofauti na badala yake ameibukia Yanga.
Tayari mchezaji huyo ameshatambulishwa ndani ya tamasha la kubwa kuliko ambalo linafanyika hivi sasa jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
Tamasha hilo linafanyika likiwa na lengo la kuanzisha harambee kubwa ya kuichangia Yanga kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
0 COMMENTS:
Post a Comment