June 11, 2019


Imeelezwa kuwa beki aliyemaliza mkataba na klabu ya KMC, Ally Ally amesema kuwa maslahi ndiyo kikwazo kilichomfanya asisaini mkataba na klabu ya Yanga.

Taarifa imeeleza kuwa Ally amedai Yanga walimpa dau dogo lililopelekea mpango huo kushindikana na sasa Beki huyo anaangalia uwezekano wa kusaini timu nyingine au kusalia KMC

"Yanga walikuja na tulikaa nao mezani shida ni dau.

"Mimi mpira ndiyo maisha yangu, siwezi kucheza kwa maslahi madogo nina ndugu wananiangalia mimi.

"Sina mkataba na timu nyingine yeyote, naendelea na mazungumzo na kuna baadhi ya timu zimenifuata."

Imeandaliwa na Yossima Sitta Jr

5 COMMENTS:

  1. Ikiwa unacho kiwango cha kupata namba basi jiunge na Mnyama na ukitakacho utakipata

    ReplyDelete
  2. kiwango gani alicho nacho wakati anapiga mpira baada ya kwenda mbele unarudi nyuma
    haha!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hakika kabisa hana kiwango cha kutingisha timu eti wafikie dau analolitaka yeye,anacheza mpira wa kawaida tu ambao hata vijana wengine kwenye ndondo cup wanaupiga au zaidi yake

      Delete
  3. Vipi washindwe na wao wana uwezo WA mchezaje yeyote wamtakae?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hivi hata kama una bilioni 10 mfukoni halafu ukawa na hitaji la kununua gari,ukakuta kuna gari ambalo unalihitaji lakini kwa mtazamo wako thamani ya gari hilo ni milioni 20 lakini muuzaji anakwambia linauzwa milioni 70.......utanunua tu kwa kuwa unazo fedha za kutosha au utataka ununue kitu kulingana na thamani yake?.....jibu rahisi ni kwamba utanunua kulingana na thamani ya gari lenyewe,ukitoa tu 70 eti kwakuwa bado utakuwa na fedha nyingi(9,930,000,000/=)basi utakuwa chizi na mpumbavu wa kwanza kati ya wapumbavu wote duniani.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic