BAADA ya Shirikisho la Soka Afrika kuthibitisha kwamba rasmi Tanzania itashirikisha timu nne michuano ya kimataifa kutokana na kukidhi vigezo hasa baada ya kushika nafasi ya 12 kwa ubora, uongozi wa Simba umetoa tamko kwa timu zitakazoshiriki.
Kuongezeka kwa timu moja kila michuano inafanya Tanzania kufikisha jumla ya timu nne ambazo kwa upande wa Ligi ya Mabingwa ni Simba na Yanga huku kwa upande wa kombe la Shirikisho ni Azam FC na KMC.
Mafanikio ya soka kwa Tanzania yamechangiwa na mabingwa hao ambao msimu uliopita walifika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika hali iliyofanya nafasi ya Tanzania kupanda kwa ubora mpaka nafasi ya 12.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa ni zamu ya timu zilizopta nafasi ya kushiriki kimataifa kupeperusha vema Bendera ya Tanzania.
" Nafasi hii adimu ambayo imeipata nchi yetu ya Tanzania ni kwa mara ya kwanza tunapeleka timu nne katika mashindano ya Caf, hivyo kwa waliopata nafasi ni muda wa kufanya kweli na sio kuturudisha tulikotoka," amesema Manara.

La msingi kama CAF imetuamini kuwa Tanzania kiwango cha soka kimepanda basi ni lazima takae chini na kutafakari tena na tena juu ya ushiriki wetu wa timu ya Taifa AFCON. Mimi kama mdau wa soka siridhishwi na mikakati ya maandizi ya timu yetu ya Taifa na nadhani tunakwenda kutia aibu Afcon. Namba moja sina imani na uwezo wa kocha wa Taifa stars kiuhalisia anabebwa na ukubwa wa Jina lake kuliko uwezo wake wa kazi katika fani ya kufundisha hasa kuiandaa timu kwenda kushiriki mashindano makubwa kama ya Afcon.lakini ukisema watu wasichopenda kukisikia hata kama ukweli unaonekana adui. Nnaimani Taifa stars kama ingekuwa chini ya kocha kama Zahera basi hii timu sasa ingelikuwepo ufaransa au ubeligiji kwa maandalizi.Na kila Mtanzania angekaa na kutulia kwatu kwa kujua kuwa kocha kiongozi yupo. Amunike ni kocha alietufelisha kwenye mechi za mchujo lakini lakushangaza tumemuachia kwenda kusimamia timu yetu ya Taifa zidi ya timu kama Senegal na Algeira wakati alishindwa kuiongoza taifa stars kupata ushindi mbele ya lethoso? Kama kweli wewe Mtanzaia kichwa chako kinafanya kazi vyema utanielewa wapi yalipo machungu yangu. Hivi sasa anaendelea na mazoezi yake magumu kwa wachezaji wa Taifa stars wakati mashindano yapo mwezi huuhuu wa sita? Nadhani wahusika wangepambana zaidi kupata mechi za kujipima nguvu za mapema zaidi kabla ya mashindano zidi ya timu kaliba ya wapinzani wetu wa Afcon ili kupata tathnini halisi juu ya uwezo wa vijana wetu kimataifa. Kusubiri mpaka wiki moja imebaki kabla ya mashindano ndio timu inacheza mechi za kujipima nguvu kutasaidia nini? na hayo mapungufu yatakayoonekana yatafanyiwa kazi ya kurekebishwa wakati gani? Tukae tusubiri maumivu. Sina wasiwasi na wachezaji wetu najua kama upangaji wa namba utakuwa sahihi basi wanaweza kufanya saprise Misri bali wasiwasi wangu upo kwenye benchi la ufundi. Bado jinamizi la goli saba mtungi za Algeria zidi ya Taifa stars ya Mkwasa huwa linanitokezea mara kwa mara usingizini. Sasa Sadio Mane na jeshi lake la ulaya huwa linaniletea kilugulia cha roho kila nikiwafikiria. Victor wanyama na jeshi lake la kambi ya ulaya kama ningekuwa mkenya nisengekuwa na presha kwani naiona Kenya ni fair matchup mbele ya vigogo hivi viwili vya soka la Africa kwenye kundi la stars. Sio kwamba tunajitisha bali ni vyema kuelewa ukubwa wa tatizo ili kuwa na tafakuri ya kutosha kupanga mbinu jinsi ya kukabiliana nalo na kama si kushinda vita basi angalau kupunguza madhara. Kuliko kuwa na mawazo yakuwa tumefuzu Afcon basi na sisi sasa tumekuwa na level moja na Egypt,Senegal na Algeria hapana na haifai kujipeleka kichwa kichwa Afcon kwani hii sio secafa lazima tujipange jamani.
ReplyDelete