June 5, 2019

BAADA ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kuongeza nafasi mbili kwa nchi ya Tanzania kushiriki michuano ya kimataifa kwa msimu wa mwaka 2019/20 na nafasi hizo mbili kuchukuliwa na Yanga pamoja na timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) Shirikisho la Soka Tanzania, TFF limefafanua sababu ya KMC kupenya kimataifa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa TFF, Cliford Ndimbo amesema kuwa maboresho ya kanuni za TFF yameipa nafasi KMC kushiriki michuano ya kimataifa.

"Kanuni zilifanyiwa maboresho ambapo nafasi ya kushiriki kombe la Shirikisho kwa timu ya pili ilikuwa ni kwa timu itakayomaliza ligi ikiwa nafasi ya tatu na kama itatokea iliyo nafasi ya tatu ikawa bingwa basi nafasi inachukuliwa na yule aliye nafasi ya nne.

"Msimu huu bingwa wa kombe la Shirikisho ni Azam FC ambaye kwenye ligi yupo nafasi ya tatu hivyo nafasi yake inachukuliwa na timu inayoshika nafasi ya nne ambayo ni KMC.

"Hivyo kama Lipuli angekuwa bingwa wa FA, nafasi hiyo ingechukuliwa na Azam FC ambao wapo nafasi ya tatu, kwa sasa timu zitakazoshiriki michuano ya kimataifa zitakuwa nne ambazo ni Simba, Yanga kwenye Ligi ya Mabingwa na Azam FC pamoja na KMC kwenye kombe la Shirikisho," amesema Ndimbo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic