MASOUD Djuma kipenzi cha mashabiki anapewa nafasi ya kutua bongo akiwa kwenye dawati la ufundi wa timu ya Manispaa ya Kinodoni 'KMC' ambayo kwa sasa ni ya kimataifa ikishiriki kombe la Shirikisho kwa mara ya kwanza.
Djuma alikuwa kocha msaidizi wa Simba alifungashiwa virago baada ya kutokuwa na maelewano na Kocha Mkuu, Patrick Aussems 'Uchebe'.
Habari kutoka ndani ya KMC zimeeleza kwamba uongozi wa KMC upo bize kumtafuta mrithi wa Ettiene Ndayiragije ambaye amebwanga manyanga moja kwa moja huku akiwa mguu nje ndani kutua Azam FC.
"Kwa sasa hakuna jambo ambalo linaendelea ndani ya KMC zaidi ya kufikiria nani atakuwa Kocha Mkuu na tayari mazungumzo kwa baadhi ya makocha yameanza ikiwa ni pamoja na Djuma aliyeionoa Simba pamoja na yule wa Lipuli," kilieleza chanzo.
Ofisa Habari wa KMC Anwari Binde amesema kuwa mchakato wa kutafuta Kocha Mkuu sio wa mchezo ni lazima utumie muda na tayari wameshapata barua za makocha wakiomba nafasi.
"Makocha wengi wametuma CV zao kuomba kazi hivyo muda ukifika kila kitu kitakuwa wazi," amesema Binde.
0 COMMENTS:
Post a Comment