June 8, 2019


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amemnasa beki wa KMC, Ally Ally huku akiibomoa Lipuli FC kwa kusajili mabeki wawili wa pembeni, Paul Ngalema na William Lucian ‘Gallas’ aliyetajwa katika usajili wa Simba.

Mkongomani huyo, hivi karibuni alitangaza kusajili wachezaji watatu wazawa pekee katika usajili wa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na kutoka nje ya nchi wakiwa sita pekee.

Kocha huyo alitarajiwa kutangaza usajili wa wachezaji atakaowasajili wapya na wale atakaowaacha mara baada ya mchezo wa mwisho wa ligi kumalizika dhidi ya Azam FC uliopigwa jana Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Kocha huyo amevutiwa na kasi na uwezo mkubwa wa mabeki hao wa pembeni Gallas na Ngalema katika kuanzisha mashambulizi na upigaji mzuri wa krosi huku wakilinda goli lao ndani ya wakati mmoja.

“Kocha anaendelea na usajili wa wachezaji wake wa nje na ndani ya nchi na zoezi hilo analisimamia yeye mwenyewe kwa kusajili wale wachezaji aliowatolea mapendekezo ya usajili.

“Uongozi huu mpya hautaki kuona kocha wao anaingiliwa na hivyo amepanga kusajili mabeki wawili wa pembeni  ambao wameonyesha uwezo mzuri mara tatu tulizokutana katika
ligi na Kombe la Shirikisho.

“Pia, beki wa kati Ally Ally ambaye amevutiwa na utulivu wake na umakini wake, hivyo mabeki hao wote watasaini mkataba mara baada ya michezo yao ya mwisho ya ligi inayotarajiwa kumalizika leo (jana),”kilisema chanzo chetu cha kuaminika.

Beki Lamine Moro wa Ghana na Mnyarwanda, Patrick Sibomana wamesaini tayari. Zahera alithibitisha hilo kuwa; “Nimepanga kusajili wachezaji watatu wazawa badala ya wawili niliyotangaza awali kati ya hao wapo mabeki wawili kutoka Lipuli (Gallas na Ngalema) na beki wa kati wa KMC (Ally Ally).”

“Katika usajili wangu huu wa wazawa sitasajili mchezaji yeyote anayecheza nafasi ya ushambuliaji zaidi ya mabeki na ninataka kusajili nafasi ya mbele wachezaji kutoka nje ya nchi pekee, hivyo tusubirie muda ukiļ¬ ka nitaweka wazi,”alisema Zahera huku akifurahia mazingira ya The Atriums Hotel iliyoko Sinza Afrikasana.

Wachezaji hao wote anaowataka Zahera ni huru wanaoruhusiwa kusaini mkataba wakati wowote kutokana na mikataba yao kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

2 COMMENTS:

  1. Mie nashauri tu kwa watani zahera apewe nafasi ya kuwa msemaji wa yanga badala ya kucoach

    ReplyDelete
  2. Hata akisajiri wote 1st eleven wa lipuli , lakini kichapo kutoka kwa kamwene bado kinamsubiri msimu ujao

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic