KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa anaogopa kufanya kazi na mzawa kwa kuwa ana mfano hai aliouona kwa kocha wa Azam FC Hans Pluijm ambaye alitimuliwa ndani ya Azam FC.
Hii ni kutokana na kile kilichoelezwa kwamba anatafutiwa kocha msaidizi ambaye atafanya naye kazi msimu ujao kwenye benchi la ufundi.
Zahera amesema kuwa alikaa na Pluijm baada ya kupigwa chini na alimwambia mambo mengi ambayo yanamtisha kufanya kazi na wazawa.
"Ujue sio kwamba sipendi kufanya kazi na wazawa hapana, najua wana uwezo na kazi wanapiga ila tatizo lipo kutokana na namna ambavyo wanawaendesha wachezaji wa ndani.
"Yule kocha wa Azam FC,(Pluijm) nilikaa naye na nikazungumza naye mengi akaniambia namna ilivyo kazi kufanya kazi na wazawa hivyo kama wao watanitafutia kocha mzawa hiy sio sawa kwangu," amesema Zahera.
0 COMMENTS:
Post a Comment