June 11, 2019

UONGOZI wa Simba umesema kuwa klabu ya Polokwane FC ya nchini Afrika Kusini imekiuka makubaliano ya FIFA kwa kudai mchezaji John Bocco ni mali yao.

Jana Simba walitoa taarifa rasmi kuhusu kumuongezea kandarasi ya miaka miwili nahodha wa kikosi hicho John Bocco ghafla wameibuka viongozi wa timu ya Polokwane wakidai mchezaji ni wao.

Polokwane wamedai kwamba Bocco alisaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo yenye maskani yake Afrika Kusini.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori amesema kuwa klabu hiyo imekiuka makubaliano ya FIFA kwa kumsainisha mkataba mchezaji mwenye mkataba.

"Hata kama mchezaji amebakisha miezi sita ni lazima klabu iandikiwe barua ili kupata taarifa, mchezaji alisema amesaini mkataba wa awali, ndio maana tukamsainisha.

"Wao hawajaandika barua kwa ajili ya kutaka kumsainisha mchezaji  Bocco, niliongea na wakala wa aliyemsainisha mkataba, hivyo niliwaambia kwamba wamekiuka makubaliano ya mkataba ndio maana hata TP Mazembe walipotaka kumsainisha mkataba Ajibu walituma barua kwa Yanga

"Huwezi kumsainisha mkataba mchezaji mwenye mkataba ndani ya mkataba hivyo hao wanaosema wamemsainisha mkataba Bocco wamekiuka makubaliano ya FIFA," amesema Magori.

4 COMMENTS:

  1. Dooooh tutaona mengi,wachezaj wanadanganyaga umri,sasa wanapodanganya na Elimu yao matokeo ndo haya tunayaona,hii Mambo huwez kukuta ulaya

    ReplyDelete
  2. Simba wangemuachia tu Boko aende zake.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni vyema wangemuacha na matatizo yake ya kukosa magoli ya wazi na kutupa presha mashabiki wa Simba.Japo ni msumbufu lakini tatizo lake ana papara si mtulivu

      Delete
    2. Nakubaliana 100 kwa 100 na wewe.. Hivi Simba kweli ni wa kumng'ang'ania huyo Bocco??
      Wamuache aende zake...
      Msahmbualiaji gani unakosa magoli hadi 5 kwenye mechi moja ili ufunge goli 1??
      Au ndo yale yale ya Morinho na Lukaku..??
      Simba gotta be serious!

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic