KOCHA SIMBA: YANGA WAMESAJILI MAJEMBE
MAMBO ni moto ndani ya Yanga. Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya usajili wa timu hiyo ilioufanya mpaka sasa kupongezwa na baadhi ya makocha wa kutoka nje ya nchi ambao wamewahi kufundisha soka hapa nchini. Mpaka sasa Yanga imewasajili wachezaji tisa wapya ambapo sita kati ya hao ni wa kutoka nje ya nchi.
Wachezaji wa nje ya nchini ni Erick Rutanga kutoka Burundi, Patrick Sibomana (Rwanda), Lamine Moro (Ghana), Issa Bigirimana (Rwanda), Maybin Kalengo (Zambia) pamoja na Farouk Shikalo (Kenya). Wazawa ni Abdulaziz Makame (Zanzibar), Ally Sonso (Lipuli FC) na kipa wa Mbao FC, Metacha Mnata.
Kutokana na usajili huyo, aliyewahi kuwa Kocha Msaidizi wa Simba, Mrundi, Masoud Djuma ameliambia Championi Jumatatu kuwa wachezaji ambao Yanga imewasajili kutokea Ligi Kuu ya Rwanda ambako yeye anafundisha soka kwa sasa, wana uwezo wa juu na amepongeza kwa usajili huo.
Wachezaji hao ni Rutanga ambaye alikuwa akiitumikia Rayon Sports, Sibomana (Mukura Victory) pamoja na Bigirimana (APR).
“Nimesikia kuwa Yanga imewasajili wachezaji hao, hakika ni usajili mzuri ilioufanya kwani wote ni wazuri na watakuwa na msaada mkubwa kwa timu hiyo.
“Wanajitambua lakini pia ni watu ambao bado wanatafuta mafanikio, kwa jinsi ninavyowafahamu niwaambie tu Yanga kuwa wamepata wachezaji wazuri kama kweli wamewasajili,” alisema Djuma.
Kwa upande wake aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Mzambia, George Lwandamina ameipongeza Yanga kwa usajili wa Moro ambaye ni beki wa kati pamoja na mshambuliaji, Kalengo ambao wao wanatokea katika Ligi Kuu ya Zambia.
Lwandamina amesema: “Ninawajua vizuri, hivyo naamini watakuwa na mchango mkubwa kwa Yanga kutokana na uwezo wao.
“Beki Lamine Moro ni mzuri kutokana na kuwa na kila kitu anachotakiwa kuwanacho beki, anajua kukaba, anajua kupambana lakini pia ana nguvu na uwezo mkubwa wa kucheza kwa kichwa mipira ya juu.
“Kwa upande wake, Kalengo yeye nimemfundisha katika timu ya Zesco, anajua kufunga kwa kutumia miguu lakini pia kichwa, vilevile anajua kumiliki mpira na ana kasi kubwa,” alisema Lwandamina.
Simba lazima wakubaliane na hali halisi juu ya usajili wa Yanga kuwani Kasi yao ya usajili ya wachezji wapya ni kasi ya Magufuli na kitendo chochote kile cha Simba kuleta madharau juu ya Yanga hii basi naiona Simba ikienda kuangukia pua msimu wa ligi ujao. Ikiwezekana hata maskauti wa Simba katika masuala ya usajili kujifunza kwa Yanga jinsi ya kuwa na maamuzi ya haraka juu ya usajili wa machezaji sahihi kwa wakati. Wakati mwengine pesa sio kila kitu bali kunahitajika watu wenye vichwa sahihi kufanya vitu sahihi.Kwa Yanga hii japo hatujaiona uwanjani lakini kwa umakini wa Zahera na Simba ile ya fowadi ya kumtegemea kagere peke yake na viungo wakabaji na beki walioruhusu goli tano back to back +4 za Mazembe +Simba iliyokubali kufungwa nje ndani na kitimu kinachopigania kushuka daraja yaani Kagera sugar kwa maoni yangu Simba licha kuchukua ubingwa lakini ilihitaji marekebisho makubwa zaidi ya Yanga kwa msimu unaofuata achilia mbali klabu bingwa Africa.Na wakati Yanga wakikamilisha usajili wao Simba ndio kwanza wao wanajadili ripoti ya kocha wao? Kana kwamba Simba wao ndio waliotoka kufanya uchaguzi wa uongozi mpya
ReplyDeleteCLUB BINGWA AFRIKA NDIO HIYO SASA TUTAONA KAMA MMEFANYA USAJILI MZURI.. AU UTAKUJA MSEMO WA KIKOSI BADO KUZOEANA!
Delete