June 4, 2019


Imeelezwa kuwa Kocha Mkuu wa klabu ya Simba akiwa zake Ubelgiji ameacha maagizo kwa bodi ya klabu ya Simba kuhusu usajili na kuboresha baadhi ya vitu kwenye bechi la ufundi la klabu hiyo.

Kwenye bechi la ufundi Aussems ameitaka bodi kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja kocha wake msaidizi Dennis Kitambi ambaye mkataba wa miezi minne umeisha.

Taarifa hiyo pia imeeleza kwenye ripoti hiyo inamtaka kocha wa makipa wa klabu hiyo Mohammed Muharami akasome ili aongeze ujuzi ikishindikana hiyo basi aletwe kocha mpya wa makipa

Aussems kama amepania vile msimu ujao ameitaka bodi ya klabu hiyo iboreshe vifaa vya mazoezi vya klabu hiyo vikiwepo viwanja vya mazoezi na ameiomba bodi ya klabu hiyo ilete mtaalamu wa viungo mpya kutoka nje anayejua aina ya tiba na chakula

4 COMMENTS:

  1. Kuhusu kocha wa makipa kocha Mkuu wa Simba yupo sahihi kwa asilimia mia moja 100%.Manula wa Simba sie yule wa Azam. Huyu wa kapwaya anafanya makosa ya kujirejea ya tena na tena na tena.La msingi Simba ni kutafuta kocha wa makipa mwenye uwezo zaidi na hivyo ndivyo alivyoagiza Ausems hizo za kusema sijui akasome zaidi ni kama vile Patrick Ausems ameona muhali kusema moja kwa moja aondoshwe labda kutokana na mahusiano mazuri ya kibinaadamu kati yake na kocha wake huyo wa makipa lakini kikazi Ausems ameshagundua kuwa kocha wake huyo wa makipa uwezo wake si wa kufundisha kipa wa kwenda kugombania ubingwa wa klabu bingwa Africa.

    ReplyDelete
  2. Sijui kwanini mupate tabu na kuna Kocha wa makipa mkenya Abdul Iddi Salim. Huyu mukimrudisha ataleta usasa.

    Maajuzi alikamisha masomo yake chini ya mwavuli wa shirikisho la kandanda la bara Asian (AFC) GK License Level 1.

    Na pia ana vyeti vya UEFA A Diploma,CAF A, CAF B na CAF C pamoja na cha shirikisho la kandanda la uholanzi KNVB (advanced Level 1,2and 3), cheti cha Tetra Brazil Certified in general coaching na vyengine kadhaa.

    Huyu ni kati ya wakufunzi mahiri wa afrika mashariki kwa makipa na Africa kwa ujumla.

    Kwa sasa ni mkufunzi wa makipa wa Sheikh Russel KC ya Dhaka nchini Bangladesh kwwnye Premier League yao.

    ReplyDelete
  3. Mwameja amesomea ukocha pia ana historia ya kuitumikia Simba kwa mafanikio

    ReplyDelete
  4. Anatakia mtu professional kama anavyeti vya daraja la juu poa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic