June 8, 2019


KOCHA wa magolikipa wa kikosi cha Yanga, Juma Pondamali amesema kuwa kikubwa kilichokuwa kinamponza mlinda mlango Klaus Kindoki kushindwa kufanya vizuri ni hofu akiwa langoni.

Kindoki ambaye ni chaguo namba moja mbele ya Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera msimu wa 2018/19 alikuwa akifanya makosa mengi ya kiufundi hali iliyofanya afungwe mabao kwenye baadhi ya michezo aliyokuwa langoni.

Mfano katika michezo ambayo alifungwa kwa makosa ya aina moja ni ule dhidi ya Mwadui FC uliochezwa uwanja wa Mwadui Complex ambapo alitema shuti alilopigiwa na Salum Ilanfya kabla ya Salum Aiyee kupachika bao, pia kwenye mchezo aliofungwa hattrick na Alex Kitenge alifanya makosa matatu ya kiufundi.

Pondamali amesema ni hofu tu ndiyo ilikuwa inamponza mlinda mlango huyo raia wa Congo.

"Ujue mlinda mlango ukiwa langoni ni lazima ujiamini, sasa Kindoki alichokuwa anafanya ni kushindwa kujiamini katika baadhi ya michezo hali iliyokuwa inasababisha anapoteza.

"Mlinda mlango ni makosa kuurudisha mpira ndani ya uwanja kama upo karibu na adui sasa yeye mpira ambao inabidi uukamate kwa mikono miwili yeye anautema kwa mikono miwili hali inayosababisha iwe rahisi kwa adui kufunga," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic