June 14, 2019


MSHAMBULIAJI wa Mwadui FC, Salum Aiyee ambaye ni namba moja kwa wazawa msimu wa 2018/19 kwa kucheka na nyavu akiwa na mabao 18 amesema kuwa washambuliaji wakali ndani ya Mwadui walimzuia asiwike kutokana na ugumu wa namba.

Aiyee amesema kuwa alianza kucheza soka akiwa na Mwadui msimu wa 2014/15 na alikuwa anaanzia benchi kutokana na kukutana na washambuliaji wenye uwezo zaidi yake.

"Mwadui kulikuwa na washambuliaji bora zaidi yangu kama Paul Nonga, Jersson Tegete, Bakari Kigedoke na Kelvin Sabato, hivyo kwa msimu wa 2014/15 ilikuwa nilazima nianzie benchi.

"Kilichonisaidia kufanya vizuri kwa sasa ni kuamini uwezo wangu na kutokata tamaa hicho ndiyo kikubwa kwani ushindani kwenye kila kazi ni haukosekani,"amesema Aiyee.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic