SIMBA MPYA UTAIPENDA, MKENYA AFUNGUKA
SIMBA imemalizana na mastaa wawili matata wa kigeni ambao mmoja ni straika na mwingine ni beki wa kushoto atakaemrithi Asante Kwasi.
Majina hao pamoja na mengine yanapaswa kuwasilishwa kwa haraka Caf kabla ya Juni 30, mwaka huu tayari kwa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mmoja wa viongozi wa Simba aliiambia Spoti Xtra jana Jumatano kwamba, wameshakamilisha ishu zote kuhusiana na wachezaji hao wawili lakini ni siri kubwa na watawafanyia utambulisho maalum.
Alisisitiza kwamba, wachezaji hao ni majembe na wana majina makubwa hivyo wakitangazwa au kutua kwenye ardhi ya Dar es Salaam kutatokea mshtuko. Lakini uchunguzi wa Spoti Xtra umebaini kwamba, straika ambaye Simba wanamficha ni Walter Bwalya wa Nkana ya Zambia.
Pia imeshamalizana na kiungo wa Gor Mahia, Francis Kahata na itasajiliwa na wachezaji watano kwenye wageni. Kocha wa Simba, Patrick Aussems amesema anataka wachezaji wapya watano wa kigeni ambao sifa yao kubwa wawe wamefanya vizuri na timu zao kwenye michuano ya kimataifa.
MKENYA AFUNGUKA
SIMBA imempiga chini beki wake mtukutu, Juuko Murshid raia wa Uganda lakini fasta tu wanamfikiria beki kutoka Zambia ambaye atabeba mikoba yake.
Simba wapo mbioni kumchukua beki huyo Mkenya, Mussa Mohammed ambaye amewaambia; “Mimi nipo, kama wao Simba watakuwa wananitaka basi waje wanifuate kwa ajili ya kuzungumza kisha tusaini mkataba.
Ninaweza kuondoka Nkana kwa sababu hakuna kitu ambacho kinanizuia lakini pia kuna vitu ambavyo vinaweza kuniondoa kwa sababu haviendi sawa.
0 COMMENTS:
Post a Comment