June 11, 2019


UONGOZI wa Mwadui FC umesema kuwa kwa sasa hesabu zao ni kusuka kikosi kipya kitakacholeta ushindani mkali msimu ujao baada ya kubaki kwenye Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Salehe Jembe, Katibu wa Mwadui, Ramadhan Kilao amesema kuwa baada ya kubaki kwenye ligi mpango wa kwanza ni kusuka kikosi upya.

"Tumenusurika kushuka daraja kutokana na kushindwa kumudu ushindani kwa msimu uliopita, kwa sasa tunaangalia namna bora itakayotufanya tuwe bora kwenye ushindani msimu ujao.

"Kikosi makini na chenye nguvu tutakuwa nacho msimu mpya hivyo mashabiki na wadau waendelee kutupa sapoti kama ambavyo walikuwa nasi bega kwa bega kwenye mchezo wetu wa playoff dhidi ya Geita," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic