MSANII wa muziki wa kizazi kipya Ally Kiba, amesema kuwa mashabiki wake na watanzania wanastahili shukrani kwa kujitoa kwa hali na mali kufanikisha zoezi la mchezo wao wa hisani uliochezwa jana uwanja wa Taifa.
Kiba alicheza jana uwanja wa Taifa na timu ya Mbwana Samatta kwenye mchezo wa hisani na timu yake ilipoteza kwa kufungwa mabao 6-3.
"Kitu kizuri kwa ajili ya kujitoa kwa jamii pia na watanzania wamejitoa na wanastahili shukrani, ni wajibu wetu kujitoa kwa ajili ya jamii ni baraka pia na jambo la kheri, sina cha kuwaambia watanzania zaidi ya shukrani," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment