June 3, 2019

KIUNGO mshambuliaji wa timu ya Simba, Said Ndemla amesema kuwa anahitaji kupata changamoto mpya msimu ujao hivyo kwa sasa anafikiria kwenda kucheza nje ya nchi msimu ujao ikishindikana atasaini hata Yanga.

Ndemla msimu uliopita amekuwa na changamoto ya kupata namba ndani ya kikosi kilichotwaa ubingwa kwa mwaka 2018/19 hali iliyofanya asionyeshe yale makeke waliyozoea mashabiki.

"Nina mpango wa kwenda kucheza nje ya nchi hivyo nasubiri kuona namna gani mipango itajipa, ila kama huko itashindikana nitazungumza na viongozi wangu wa Simba kama watahitaji kuongeza mkataba nami nitasaini hata Yanga pia endapo watakidhi masharti na vigezo," amesema.

Ndemla amekuwa akihusishwa kujiunga na Yanga na uongozi wa Yanga umesema kuwa suala la usajili lipo mikononi mwa kocha Mwinyi Zahera.

4 COMMENTS:

  1. Maneno yamekua mengi sana,hebu tuambie ukweli,yanga wanasema hawana haja yako

    ReplyDelete
  2. Afikiriwe mapenzi yake juu ya Simba ni yawwazi na Pia awe anaepewa fursa kila itapowezekana kwani ndio njia pekee ya kurejesha kiwango name Ndemla asivunjike moyo ajitahidi kunyanyuwa kiwango chake kama alivofanya Haruna ambaye alighibu muda mrefu lakini alijitahidi na atazame matunda ya juhudi zake

    ReplyDelete
  3. Ndemla kama ameshindwa changamoto za Simba za nje ataziwezaje? Naona Yanga na Simba zinatumiwa na wachezaji pamoja na mawakala wao kulazimisha mslahi yao kwenye vilabu hivi kwa maneno badala ya vitendo kwenye dimba .kama kweli Ndemla na wanaomshauri vichwa vyao vinafanya kazi basi wangemshauri Ndemla kwenda Azam kwani nafasi ya kucheza kimataifa ipo hata maslahi ni ya uhakika huko Yanga anachokwenda kukitafuta kitu gani? Lakini la msingi zaidi wazungu si wapumbavu na hawana kumdekeza mtu hawa akina Ndemla na wenzake pale Simba wanaweza kuona kama wanaonewa kwa kutopata nafasi za kucheza katika kikosi cha kwanza ila ikitokezea Ndemla anamkalisha benchi kotei au chama au hata mkude basi sidhani kama atakwenda ulaya kufanya majaribio akafeli.kwa bahati nzuri Simba itawakilisha Taifa tena Africa kwa hivyo hawa akina Dilunga,Mzamiru, Ndemla na wengine wengi wachezaji wazawa pale Simba ambao bado umri unawaruhusu huu ni wakati kujiandaa. Kutathmini kwanini haukuwa na msimu mzuri ligi iliyopita. Nini kilikukwamisha na nini cha kufanya ili uwe bora zaidi mwakani kwani Simba ni fursa msikubali kuondoka kirahisirahisi. Siku zote mwanaume anaezamiria kupata mafanikio ni yule anaesimama kidete bila ya kuyumba kukabiliana na changamoto zenye nia ya kumkatisha tamaa.Wahenga wanasema kazi yeyote ni mtihani mkubwa kwenye maisha kwakuwa kazi ndio maisha yenyewe na ukizembea kunako kazi yako basi werevu watanufaika na kazi yako na kuishi maisha yako wakikuacha na unyonge wako ukilalama.

    ReplyDelete
  4. Ama kwakuwa awaombe Yanga wamchukuwe ajue amejidhalilisha na watamchukuwa Kwa bei Chee huenda hata ikawa milioni nne au tatu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic